Mazuwaru wanahuisha usiku wa Ijumaa mbele ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Mji mtukufu wa Karbala umeshuhudia idadi kubwa ya mazuwaru waliokuja kuhuisha usiku wa Ijumaa mbele ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), sambamba na kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa Imamu Ali Ridhwa (a.s).

Mji wa Karbala hupokea idadi kubwa ya watu wanaokuja kufanya ziara katika malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuhuisha utiifu wao kwa Ahlulbait (a.s).

Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa mkakati maalum wa kuhudumia mazuwaru na kukidhi mahitaji yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: