Wahudumu wa kitengo cha kusimamia haram tukufu na idara ya masayyid wameshiriki katika kugawa pipi (halwa), malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) imeshuhudia idadi kubwa ya mazuwaru waliokuja kuadhimisha tukio hilo.
Tukio hilo ni sehemu ya juhudi za Atabatu Abbasiyya tukufu, za kuimarisha mafungamano ya kiroho na kijamii kwa mazuwaru, sambamba na kuimarisha mapenzi na utiifu kwa Ahlulbait (a.s) kupitia matukio ya kidini.







