Ataba mbili tukufu zinaadhimisha historia ya Imamu Ridhwa (a.s) katika kumbukumbu ya kuzaliwa kwake

Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, zinaadhimisha historia ya maisha ya Imamu Ali bun Mussa Ridhwa (a.s) katika kumbukumbu ya kuzaliwa kwake.

Limefanywa hilo katika ujumbe wa Ataba mbili tukufu uliotolewa na rais wa kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya Shekhe Swaalahu Karbalai, kwenye hafla iliyofanywa katika uwanja wa mlango wa qibla ya Abulfadhil Abbasi (a.s) wakati wa kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa Imamu Ridhwa (a.s).

Shekhe Karbalai ameongea kuhusu historia ya Imamu Ridhwa (a.s) kwenye Nyanja ya Akhlaq, Ibada na maisha yake yote kwa ujumla, akakumbusha namna alivyo zaliwa Imamu (a.s).

Akaeleza mwenendo aliokuanao Imamu Ridhwa (a.s), akasema kuwa ni mfumo kamili wa maisha ya mwanadamu katika Nyanja zote, pamoja na mazingira magumu yaliyokuwepo katika zama zake.

Kisha akaeleza hatua za maisha ya Imamu (a.s) na nafasi yake pamoja na changamoto alizopambana nazo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: