Kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kimejadili njia za kushirikiana katika sekta ya maktaba na idara ya ufundi katika mkoa wa Nainawa.
Mkuu wa kituo cha faharasi na kupangilia taaluma Sayyid Hasanaini Mussawi amesema “Kutokana na wito wa mkuu wa Maahadi idara ya ufundi kaskazini ya mkoa wa Nainawa Dokta Majidi Muhammad Swalehe, tumetembelea Maahadi na kujadili njia za kushirikiana kwenye sekta ya maktaba”.
Akaongeza kuwa “Tumeongea na mkuu wa Maahadi na rais wa kitengo cha maktaba, ustadh Aadil Abdullah uwezekano wa kunufaika watumishi kwa kupewa mafunzo kupitia semina na warsha mbalimbali zinazoandaliwa na kituo, ambazo hulenga kujenga uwezo katika sekta ya faharasi, usanifu wa machapisho na uratibu wa idara za maktaba”.