Atabatu Abbasiyya imepokea bendera ya kubba la malalo ya Bibi Maasuma (a.s)

Atabatu Abbasiyya imepokea bendera ya kubba la malalo ya Bibi Fatuma Maasuma (a.s) kutoka kwa ugeni wa malalo hiyo takatifu.

Ugeni huo umepokewa na rais wa kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Muhammad Ali Azhar.

Wageni wamefanya ziara katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kisha wakaishukuru Atabatu Abbasiyya tukufu kwa mapokezi mazuri waliyopewa.

Ni kawaida ya kila mwaka katika kuadhimisha mazazi ya Maimamu (a.s), watumishi wa malalo yao kutoa zawadi ya bendera ya muhusika kwenye Ataba zingine.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: