Muheshimiwa Sayyid Swafi amesisitiza kusaidia juhudi yeyote ya kielimu katika tafiti za Ulumul-Qur’ani

Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya, Muheshimiwa Allamah Sayyid Ahmadi Swafi amehimiza kusaidia juhudi za kielimu katika somo la Ulumul-Qur’ani.

Ameyasema hayo alipompokea mtafiti Dokta Hussein Ali Hussein, muandishi wa kitabu cha (Sunna za historia katika Qur’ani tukufu), kitabu hicho kimeandika uchambuzi wa riwaya za kiislamu katika tafsiri na historia ya kiislamu.

Akasema kuwa, anaetaka kufahamu Qur’ani tukufu bila kupitia kwa Ahlulbait (a.s) atakutana na vikwazo vingi.

Akafafanua kuwa, lazima kwa mtu anaefanya mazingatio katika Qur’ani afuate mwenendo wa aya za Qur’ani kwa kujipamba na elimu za Ahlulbait (a.s), ili apate uwelewa kamili wa aya hizo, kwani vitu viwili hivyo havitofautiani hadi siku ya kiyama kama isemavyo hadithi ya vizito viwili.

Muheshimiwa amesisitiza kusaidia juhudi yeyote ya kielimu katika somo la Ulumul-Qur’ani, ili kuwapa moyo watafiti wa somo hilo na kuwafanya waendelee na safari ya kielimu.

Dokta Hussein Ali amesema: Hakika kitabu hiki nimejaribu kuangazia michango ya wanazuoni waliotangulia na watafiti wa kiislamu kuhusu historia ya Qur’ani tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: