Atabatu Abbasiyya inaendelea na utekelezaji wa hatua ya pili katika upanuzi wa eneo la mlango wa Baghdad

Watumishi wa Ataba tukufu wanaendelea kutekeleza hatua ya pili ya mradi wa upanuzi wa eneo la mlango wa Baghdad.

Mjumbe wa kamati ya uvunjaji na upanuzi katika Ataba tukufu Sayyid Hassan Ali Abdulhussein amesema “Watumishi wetu wanaendelea na kazi za hatua ya pili katika mradi wa upanuzi, kwa kushirikiana na kitengo cha miradi ya kihandisi pamoja na vitengo vingine”.

Akaongeza kuwa “Kazi imehusisha ubomoaji wa jengo la nne miongoni mwa majengo yanayomilikiwa na Ataba tukufu katika eneo hilo”.

Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia mradi wa upanuzi wa maeneo yanayozunguka malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), inalenga kuongeza uwezo wa kupokea idadi kubwa ya mazuwaru na kurahisisha matembezi yao wakati wa ziara zinazohudhuriwa na mamilioni ya watu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: