Ustadh wa hauza Allamah Sayyid Ahmad Swafi ametoa muhadhara wa kielimu wa kila wiki katika kusherehesha dua ya Abihamza-Thamali

Ustadh wa hauza Allamah Sayyid Ahmadi Swafi, ametoa muhadhara wa kielimu wa kila wiki katika kusherehesha dua ya Abihamza-Thamali, mbele ya viongozi wa Atabatu Abbasiyya, wahudumu wake na wanafunzi wa masomo ya Dini.

Muhadhara huo ni sehemu ya mfululizo wa mihadhara ya kusherehesha dua ya Abihamza-Thamali iliyopokewa na Imamu Sajjaad (a.s).

Amefafanua kipengele kisemacho (Mola wangu nisamehe pale zinapoisha hoja zangu, na ulimi wangu utakaposhindwa kukujibu, na akili yangu itakaposhindwa kuelewa maswali yako, ewe ambae matarajio yangu kwako ni makubwa, usinitupe pindi takapozidiwa na matatizo…).

Sayyid Swafi ameongea baadhi ya riwaya zinazoeleza umuhimu wa dua na kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu mtukufu kwa kumtegemea, akasisitiza kuwa muumini anaemuomba Mwenyezi Mungu wakati wa raha anaweza kuwa bora kuliko muumini anaemuomba Mwenyezi Mungu wakati wa shida tu, wakati wa raha daima atamshukuru Mwenyezi Mungu na kumshukuru kwa neema aliyompa.

Akasema kuwa Mwanaadamu anahitaji rehema za Mwenyezi Mungu wakati wote, Mwanaadamu anaweza kutaja shida zake wakati wa dua, pamoja na kwamba Mwenyezi Mungu anatambua mambo yaliyofichikana na yaliyopo katika nafsi, mahitaji ya waja wake, lakini anapenda kusikia sauti ya mja wake ikimuomba.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: