Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, inafanya mradi wa semina za kiangazi mwaka 2025 kwa ushiriki wa wanafunzi elfu kumi kutoka maeneo tofauti ya mkoa wa Baabil.
Kiongozi wa Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Baabil chini ya Majmaa, Sayyid Muntadhiru Mashaikhi amesema “Mradi umewekwa pande zote za mkoa, kuanzia makao makuu ya mkoa hadi vijijini, kaskazini, kusini, mashariki na magharibi, chini ya walimu mahiri zaidi ya 320”.
Akaongeza kuwa “Semina haziishii kwenye kufundisha usomaji sahihi wa Qur’ani peke yake, bali zinahusisha masomo mengine pia kama Fiqhi, Aqida, Akhlaq, Sira pamoja na kuhifadhi juzu la mwisho katika Qur’ani tukufu”.
Mradi huu ni sehemu ya mkakati wa Atabatu Abbasiyya tukufu wa kujenga uwelewa wa kidini katika jamii na kunufaika na likizo za kiangazi kwa kutoa mafunzo hayo matukufu.