Atabatu Abbasiyya tukufu imekamilisha ushiriki wake katika maonyesho ya vitabu kimataifa jijini Tehrana awamu ya 36.
Ataba imewakilishwa na vitengo vyake tofauti, kitengo cha habari na utamaduni, kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu, taasisi ya utafiti Alwaafi na Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu.
Atabatu Abbasiyya imeshiriki ikiwa na machapisho zaidi ya 350, yamehusisha vitabu vya Dini, fikra, utamaduni, mausuaat pamoja na machapisho yanayo onyesha mafanikio ya vitengo na vituo vya Ataba.
Tawi la Ataba tukufu limepata muitikio mkubwa kutoka kwa wadau wa maonyesho, limetembelewa na idadi kubwa ya viongozi wa kidini na kitamaduni, jambo ambalo limesaidia kutoa fursa ya kubadilishana uzowefu.
Ushiriki huo ni sehemu ya juhudi za Atabatu Abbasiyya tukufu za kusambaza fikra za Ahlulbait (a.s) na elimu zao kwenye matukio ya kimataifa.