Marjaa-Dini mkuu Muheshimiwa Sayyid Ali Husseini Sistani, amekutana na wajumbe wa kongamano la kimataifa kutoka taasisi ya Ain na amepongeza nafasi yao kijamii na kibinaadamu.
Wageni hao wamesikiliza maelekezo ya Muheshimiwa Marjaa-Dini mkuu na nasaha zake kuhusu kuboresha kazi za kibinaadamu, amepongeza kazi nzuri wanayofanya ya kuhudumia mayatima na watu wenye mahitaji, akasema ataendelea kusaidia, akahimiza kazi za taasisi ziendelee kuwa za kibinaadamu, akawataka wahudumu wa taasisi hiyo wafanye kazi kwa bidii kufanikisha swala hilo.
Wajumbe hao wamemshukuru sana Muheshimiwa kwa kuendelea kuwasaidia, wameahidi kuzingatia maelekezo yake na kuyafanyia kazi kwa kupanua huduma zao, ili kuwafikia mayatima wengi zaidi na watu wenye mahitaji kutoka sehemu tofauti za dunia.