Kitengo cha mafundi wa majengo ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya kimekamilisha hatua ya pili ya uwekaji wa maraya katika eneo lenye pambo (sega) ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Kiongozi wa kitengo cha maraya Sayyid Hassan Saidi amesema “Watumishi wetu wamekamilisha hatua ya pili ya uwekaji wa maraya kwenye dari linalobeba pambo la haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) lenye ukubwa wa mita 80 za mraba”.
Akaongeza kuwa “Kazi imehusisha kuondoa maraya zilizoharibika, sambamba na kuzingatia nakshi maalum za maraya za dari hilo”.
Akabainisha kuwa “Kazi hiyo imefanywa na raia wa Iraq, wameweka maraya zenye upana wa milimita 2, wamefanya kazi kwa umakini na umaridadi mkubwa”.
Maraya huwekwa kwa kuzingatia maumbo, maraya zilizowekwa zinaubora wa hali ya juu na zinatoka katika viwanda bora duniani.