Atabatu Abbasiyya tukufu imekemilisha semina ya kuwajengea uwezo watumishi wapya 40 katika majengo ya Shekhe Kuleini.
Makamo rais wa kitengo cha Dini katika Ataba tukufu Shekhe Aadil Wakili amesema “Semina imedumu kwa muda wa siku tisa, jumla ya watumishi 90 wameshiriki, wamefundishwa mambo mbalimbali, wamefanya mitihani mwishoni mwa semina, jambo hilo linawasaidia kulinda elimu zao na kunufaika nazo wakati wa utendaji wao”.
Akaongeza kuwa “Kitengo cha Dini husaidia kufundisha kwenye semina mbalimbali, kimefundisha somo la Fiqhi, Aqida na Akhlaq, sambamba na kugawa vijitabu kutoka kwa Marjaa-Dini mkuu Muheshimiwa Sayyid Ali Husseini Sistani na kitabu cha Aqida kilichoandikwa na Shekhe Twariq Albaghdad”.
Akafafanua kuwa “Kitengo cha kulinda nidham katika Atabatu Abbasiyya, kinanafasi kubwa ya kuratibu semina hii”, tambua kuwa watumishi watakao faulu mitihani yao watapewa vyeti.