Ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) asubuhi ya Ijumaa, umeshuhudia usomwaji wa Dua Nudba uliohudhuriwa na kundi kubwa la mazuwaru.
Dua imesomwa katika mazingira tulivu kwa ushiriki wa mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu huandaa mazingira mazuri ya usomaji wa dua, huweka vitabu vya dua, huandaa sehemu maalum ya kufanyia ibada hiyo na kutoa huduma za lazima kwa mazuwaru.