Ustadh wa hauza Allamah Sayyid Ahmadi Swafi, ametoa muhadhara wa sita katika kusherehesha dua ya Abihamza Thamali, mbele ya viongozi wa Atabatu Abbasiyya, wahudumu na wanafunzi wa Dini.
Muhadhara huo ni muendelezo wa mihadhara inayotolewa na muheshimiwa katika kusherehesha dua ya Abihamza Thamali iliyopokewa kutoka kwa Imamu Sajjaad (a.s).
Muheshimiwa amefafanua aya za Qur’ani, hadithi za Mtume na vipande vya dua hiyo kutoka kwa Imamu (a.s), vinavyo engelea siku ya kiyama, na hatima ya mauti hadi kwa wasioamini akhera, kama vile makafiri na watu wengine wa mfano wao, pamoja na kukataa kwao siku ya ufufuo, lakini mwanaadamu akitafakari kwa makini atatambua kuwa lazima atafufuliwa.
Muheshimiwa akasema kuwa Imamu (a.s) anasoma dua na anatuambia kuhusu Qur’ani tukufu yatakayojiri katika moto wa Jahannam, na yatakayotokea kwa watu watakaokaa motoni milele na wanafiki, bila kusahau waumini watakaofaulu kukaa peponi, uwepo wa itikadi hizi kwa mwanaadamu kunamfanya akumbushe nafsi yake wakati wote na kumsaidia kupata msimamo, hadithi tukufu zinamsaidia mwanaadamu anaejitambua na kujipa mawaidha ndani ya nafsi yake.
Akabainisha kuwa mwanaadamu hajawahi kuona akhera lakini anasikia kuhusu akhera kupitia aya tukufu za Qur’ani, hivyo tunaweza kuona picha anayotupa Imamu (a.s), akasema huo ndio ubora wa Maimamu watakatifu (a.s) kumfanya mwanaadamu achukue tahadhari.
Kwa ziada fungua link ifuatayo: https://www.youtube.com/watch?v=6TvfixK6Y-M