Kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya kimesema kuwa, kinagawa maji ya baridi na barafu muda wote kwa mazuwaru wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kufuatia kuingia msimu wa joto.
Makamo rais wa kitengo hicho Sayyid Abbasi Mussawi amesema “Kitengo kinaendelea kuhudumia mazuwaru wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kupitia idara zake tofauti”, akabainisha kuwa “Idara ya maji kufuatia kuingia msimu wa kiangazi na kuongezeka kiwango cha joto, imeanza kugawa maji ya baridi na barafu kwa mazuwaru wa malalo takatifu muda wote”.
Akaongeza kuwa “Kitengo kinamiliki viwanda viwili vya kutengeneza barafu, ambavyo ni kiwanda cha Alqami kilichopo eneo la mlango wa Kibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na kiwanda cha Furaat kilichopo karibu na Maqaam ya Imamu wa zama (a.f), vinazaliwa mifuko 300 ya barafu kwa saa moja, ambayo hutolewa bure kwa mawakibu Husseiniyya na wananchi”.
Akaendelea kusema kuwa “Idara ya maji inagawa maji baridi ya kunywa kwa mazuwaru kupitia deli za maji zilizowekwa kwenye barabara zinazoelekea haram takatifu”.