Atabatu Abbasiyya imeweka mabango yanayo ashiria huzuni kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu kufuatia kumbukumbu ya kifo cha Imamu Aljawaad (a.s)

Watumishi wa kitengo kinachohudumia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu katika Atabatu Abbasiyya, wameweka mabango yanayo ashiria huzuni katika kuomboleza kumbukumbu ya kifo cha Imamu Muhammad Aljawaad (a.s).

Mabango hayo yameandikwa maneno yanayo bainisha dhulma alizofanyiwa Imamu Aljawaad (a.s) na sifa zake.

Jambo hilo ni sehemu ya juhudi za Ataba tukufu katika kuonyesha muonekano wa huzuni, utiifu na mapenzi kwa Ahlulbait (a.s).

Atabatu Abbasiyya huadhimisha matukio yanayo husu Ahlulbait (a.s) likiwepo hili la kumbukumbu ya kifo cha Imamu Muhammad Aljawaad (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: