Ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), umeshuhudia tukio la kiibada lililofanywa na watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika kuomboleza kifo cha Imamu Muhammad Aljawaad (a.s).
Tukio hilo limehusisha usomaji wa ziara ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wimbo wa (Lahnul-Iba), qaswida na tenzi kuhusu kifo cha Imamu Muhammad Aljawaad (a.s) kwa ushiriki wa kundi kubwa la mazuwaru.
Wahudumu wa Atabatu Abbasiyya hufanya tukio la kiibada siku ya Jumatatu na Alkhamisi kila wiki.