Makundi ya waombolezaji katika mji wa Kadhimiyya, yamehuisha usiku wa kumbukumbu ya kifo cha Imamu Muhammad Aljawaad (a.s) mbele ya kaburi lake takatifu.
Mji wa Kadhimiyya umepokea idadi kubwa ya mazuwaru waliokuja kuhuisha usiku wa ishirini na tisa katika mwezi wa Dhulqaadah, ambao ni usiku wa kumbukumbu ya kifo cha Imamu Aljawaad (a.s).
Atabatu Abbasiyya inahudumia mazuwaru kupitia maukibu maalum siku zote za uombolezaji na ziara hiyo tukufu.