Idara ya Fatuma binti Asadi imeomboleza kifo cha Imamu Aljawaad (a.s)

Idara ya Fatuma binti Asadi (a.s) ya masomo ya Qur’ani chini ya ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya, imeomboleza kifo cha Imamu Muhammad Aljawaad (a.s).

Idara imeandaa majlisi ya kuomboleza iliyofanywa kwa ushiriki wa wanafunzi wa semina ya (Yanabia-Rahmah) awamu ya pili, imejikita katika kueleza historia ya Imamu Muhammad Aljawaad (a.s) na nafasi yake katika kuongoza umma.

Majlisi ikahitimishwa kwa kusoma qaswida na tenzi katika mazingira yaliyojaa huzuni na majonzi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: