Wahudumu wa Ataba mbili wameomboleza kifo cha Imamu Aljawaad (a.s) kupitia maukibu ya uombolezaji ya pamoja

Wahudumu wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya wameomboleza kifo cha Imamu Muhammad Aljawaad (a.s) kupitia maukibu ya pamoja.

Maukibu hiyo imehudhuriwa na wajumbe wa kamati kuu ya uongozi katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Kadhim Abadah, Dokta Afdhalu Shami, mkuu wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Jawadi Hasanawi na viongozi wengine.

Shami amesema “Wahudumu wa Ataba mbili tukufu wanautamaduni wa kuhuisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s) kipindi chote cha wamaka, likiwemo tukio huli la kuomboleza kifo cha Imamu Muhammad Aljawaad (a.s), kupitia maukibu ya pamoja”.

Maukibu imeanza matembezi yake katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wakipitia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, hadi kwenye malalo ya Imamu Hussein na kumpa pole kutokana na msiba huu, waombolezaji wameimba qaswida na tenzi za kuomboleza zilizoamsha hisia za huzuni na majonzi katika nyoyo za waumini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: