Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake chini ya ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya imeomboleza kifo cha Imamu Muhammad Aljawaad (a.s).
Majlis imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, ikafuatiwa na ziara maalum ya Imamu Aljawaad (a.s), kisha igizo lenye anuani isemayo (Na wakamuuwa mtunza rehema), limeangazia maisha ya Imamu (a.s), likifafanua dhulma alizofanyiwa, utukufu wake na hekima zake.
Majlis imefanywa katika jengo la Swidiqatu Twahirah (a.s), imehitimishwa kwa qaswida na tenzi za kuomboleza katika mazingira yaliyojaa huzuni na majonzi.