Jumuiya ya Al-Ameed imetoa wito kwa watafiti kuhudhuria kongamano la kielimu na kitamaduni kuhusu fatwa tukufu ya kujilinda awamu ya sita.
Kongamano litafanywa chini ya usimamizi wa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, nalo ni sememu ya kongamano kubwa la fatwa ya kujilinda awamu ya tisa, linalofanywa chini ya kauli mbiu isemayo (Marjaa-Dini mkuu ni ngao ya umma wa kiislamu) na anuani isemayo (Fatwa tukufu ya kujilinda baina ya muda uliopita na sasa Maraajii wawili Muheshimiwa Sayyid Sistani na muheshimiwa Shekhe Jafari Kaashifu Alghitwaa, malengo yanafanana na njia zinatofautiana).
Kongamano litafanywa kwa ushirikiano wa chuo kikuu cha Alkafeel, Al-Ameed, na kitivo cha Fiqhi katika chuo kikuu cha Kufa Ijumaa ya kesho tarehe 30/5/2025 saa nane mchana katika ukumbi wa Imamu Hassan Almujtaba (a.s) ndani ya Ataba tukufu.