Atabatu Abbasiyya imeonyesha filamu ya fatwa ya kujilinda

Shughuli za kongamano la fatwa ya kujilinda awamu ya tisa, zimepambwa na filamu ya fatwa ya kujilinda na vita vya ukombozi pamoja na kuonyesha baadhi ya watu waliouawa kishahidi katika vita hiyo.

Kongamano linafanywa chini ya kauli mbiu isemayo (Marjaa-Dini ni ngao ya umma wa kiislamu), limeratibiwa na kitengo cha habari na utamaduni kwa kushirikiana na taasisi ya uhakiki na utafiti Alwaafi chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Filamu imetengenezwa na taasisi ya Alwaafi, inavipande vya khutuba za Ijumaa kutoka kwa muwakilishi wa Marjaa-Dini mkuu katika mkoa mtukufu wa Karbala, vipande vya vita ya ukombozi na watu waliouawa kishahidi.

Filamu hiyo ni sehemu ya uthibitisho wa namna raia wa Iraq walivyo itikia wito wa fatwa tukufu ya kujilinda na jinsi walivyo jitolea, aidha ni mradi wa kutunza kumbukumbu sahihi na kulinda zisipotoshwe.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: