Hafla ya mwisho katika tamasha la kimalezi linalofanywa na shule za Al-Ameed mwaka 2025 imepambwa na filamu yenye anuani isemayo (Hadithi huanzia utotoni mwetu).
Hafla imesimamiwa na kitengo cha malezi na elimu katika Atabatu Abbasiyya chini ya kauli mbiu isemayo (Upande wa mwezi imepandwa ikamwakiliwa na kutoa matunda), mbele ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Muheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, katibu mkuu Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini, baadhi ya wajumbe wa kamati kuu, viongozi wengine wa Ataba, viongozi wa kisekula na familia za watoto.
Filamu inahusisha maonyesho ya mahojiano ya viongozi wa kitengo wakiongelea hatua za mradi wa malezi, ambao unasehemu tatu, sehemu ya kwanza inahusisha uwepo wa watalamu wa malezi wanaotoa mafunzo kwa watoto, sehemu ya pili inaelezea mfumo wa (upande wa mwezi), sehemu ya tatu inaeleza namna kitengo cha malezi na elimu kinavyo tumia mifumo ya kisasa katika kutafuta mafanikio.
Aidha filamu inavipengele vingi vinavyo onyesha mahojiano na wazazi wa wanafunzi, ili kubainisha uwelewa wa mradi na namna unavyo changia kuendeleza watoto wao.