Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake chini ya ofisi ya kiogozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya, inafanya mitihani ya muhula wa pili kwa wanafunzi wa Maahadi ya uhadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake.
Siku ya Jumamosi mwezi 3 Dhulhijjah, idara imefanya mtihani wa kwanza wa muhula wa pili katika mwaka wa masomo 1446h kwenye Maahadi ya wahadhiri wa Husseiniyya chini ya usimamizi wa walimu na viongozi.
Kiongozi wa idara bibi Taghridi Tamimi ametoa khutuba elekezi kwa wanafunzi muda mfupi kabla ya kuingia kwenye kumbi za mitihani, amesisitiza umuhimu wa kujifunza mwenendo wa Ahlulbait (a.s) na kufanya jambo kwa bidii huleta mafanikio.
Mitihani husaidia kuboresha kiwango cha elimu kwa wanafunzi na huwaandaa kuelndelea na hatua za masomo zinazofuata.