Kumbukumbu ya ndoa ya nuru mbili.. Idara ya Fatuma binti Asadi imefanya semina ya (Niunganishe na wema)

Idara ya Fatuma binti Asadi (a.s) ya masomo ya Qur’ani chini ya ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya imefanya semina yenye anuani isemayo (Niunganishe na wema) kukumbuka ndoa ya nuru mbili Imamu Ali na Bibi Fatuma Zaharaa (a.s).

Uongozi wa idara umesema kuwa semina imehusisha mabinti wanaohifadhi kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu, imekua na mazingira ya pekee kwa washiriki, akasema kuwa muda wa semina hiyo umeenda sambamba na kumbukumbu ya ndoa ya nuru mbili, ili kuonyesha mahusiano makubwa baina ya Qur’ani na Ahlulbait (a.s).

Akaongeza kuwa semina imefunguliwa kwa kutambulisha mradi na malengo yake, pamoja na kusisitiza umuhimu wa kuhifadhi Qur’ani tukufu na kueleza nafani ya mtu aliyehifadhi Qur’ani, sambamba na kufafanua mbinu na njia zinazorahisisha kuhifadhi.

Idara ikafafanua kuwa, ratiba yake katika kuhifadhisha Qur’ani inagusa makundi tofauti ya umri, ndani ya kipindi cha mwaka hupokea idadi kubwa ya washiriki wa semina za Qur’ani ambazo huhusisha watu wenye umri na viwango tofauti, kwa lengo la kujenga uwelewa wa Qur’ani tukufu katika nafsi zao na kuifanya kuwa mfumo wa maisha.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: