Kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kimetoa wito wa kushiriki kwenye nadwa iliyopewa jina la (Athari za Hijja na turathi za kiislamu kwa waafrika).
Nadwa inasimamiwa na Markazi Dirasaati Afriqiyya, wahadhiri wa nadwa hiyo ni mkuu wa kitivo cha adabu katika chuo kikuu cha kiislamu cha Minnesota nchini Marekani Dokta Swalehe Maharusi, Dokta Nizaar Alwaani kutoka kitivo cha malezi katika chuo kikuu cha Mustanswiyya, Dokta Muhammad Arifi kutoka kitivo cha adabu na masomo ya kiislamu tawi la chuo kikuu cha Minnesota cha Marekani nchini India.
Nadwa itafanywa kesho siku ya Jumanne tarehe (3/6/2025) saa mbili jioni kupitia jukwaa la Google Meet.