Mkuu wa Maahadi Shekhe Waailiy na Shekhe Faisal Alkaadhimi wamesema: “Majlisi imejikita katika kueleza sekta kuu tatu kuhusu maisha ya Imamu Albaaqir (a.s), sekta ya elimu, Jamii na mambo yanayofungamana na Karbala”.
Akaongeza kuwa “Kila tukio linamafundisho na mazingatio mengi, tunajifunza mambo mengi kutoka katika maisha ya Imamu Albaaqir (a.s), miongoni mwa mambo hayo ni, kukemea ukatili, kujenga uelewa, ikhalasi katika kazi, elimu na utamaduni”.
Atabatu Abbasiyya tukufu huomboleza vifo vya Maimamu wa Ahlulbait (a.s) kwa kuandaa ratiba kamili ya uombolezaji, inayohusisha kufanya majlisi na kuhudumia mazuwaru.