Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake chini ya ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya imefanya nadwa kuhusu Imamu Muhammad Jawaad (a.s).
Kiongozi wa Maahadi Bibi Manaar Aljaburi amesema “Maahadi imefanya nadwa kuhusu Imamu Jawaad (a.s) kujikumbusha nafasi yake tukufu na misimamo yake”, nadwa imehudhuriwa na wanafunzi 200 kutoka mradi wa semina za Qur’ani katika majira ya kiangazi”.
Akaongeza kuwa “Nadwa imeangazia kauli ya Imamu Jawaad (a.s) katika kubainisha maana ya ushia kwa kauli na vitendo, ikiwemo na uwelewa wa kusubiri faraja”