Kitengo cha Dini kimetoa muhadhara wa kuomboleza kifo cha Imamu Albaaqir (a.s)

Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya kimefanya muhadhara wa kuomboleza kifo cha Imamu Muhammad Baaqir (a.s) katika haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Muhadhara umetolewa na rais wa kitengo hicho Shekhe Swalahu Karbalai, ametaja historia na msimamo wa Imamu Baaqir (a.s) kufuatia kumbukumbu ya kifo chake.

Shekhe ameeleza sehemu ya maisha ya Imamu (a.s), dhulma alizofanyiwa, msimamo wake katika kulinda misingi ya Dini na kusambaza elimu na maarifa ya kiislamu.

Utoaji wa muhadhara ni sehemu ya ratiba ya kitengo katika kuadhimisha matukio ya kidini, jambo hilo lina athari kubwa katika kujenga uelewa wa itikadi na kuimarisha kufungamana na Maimamu (a.s).

Atabatu Abbasiyya tukufu hutoa mihadhara ya kidini kwa lengo la kujenga uwelewa kwa mazuwaru na kuhuisha mafundisho ya Ahlulbait (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: