Atabatu Abbasiyya imefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Muslim bun Aqiil (a.s) katika ukumbi wa utawala.
Mhadhiri wa majlisi alikuwa ni shekhe Ali Dujaili, ameongea historia tukufu na msimamo madhubuti aliokua nao balozi wa Imamu Hussein Muslim bun Aqiil (a.s).
ameeleza sehemu ya maisha yake na nafasi yake katika kujenga misingi ya Dini na namna alivyo utendea haki ujumbe wa Imamu Hussein (a.s) kwa watu wa Karbala.
Majlisi za kuomboleza katika Ataba tukufu ni sehemu ya kuhuisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s) na wafuasi wao.