Kundi kubwa la waumini limeswali swala ya Idhul-adh-ha ndani ya ukumbi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Swala ya Idul-adh-ha imeswaliwa zaidi ya mara moja ndani ya ukumbi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kutokana na idadi kubwa ya waumini waliojitokeza kutoka ndani na nje ya mkoa wa Karbala.
Waumini wamemuomba Mwenyezi Mungu mtukufu alitunuku Amani na usalama taifa la Iraq, awarehemu mashahidi na kuwaponya haraka majeruhi na wagonjwa.
Vitengo vya Atabatu Abbasiyya vimeweka mkakati maalum wa kutoa huduma bora kwa mazuwaru wa Abulfadhil Abbasi (a.s).