Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya amepokea watu wanaokuja kutoa pongezi za sikukuu ya Idhul-adh-ha

Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini amepokea watu wanaokuja kutoa pongezi za sikukuu ya Idul-adh-ha.

Katika kupokea wageni wanaokuja kutoa salamam za Iddi wameshiriki pia wajumbe wa kamati kuu na marais wa vitengo, wamepeana pongezi na kutakiana heri na Baraka.

Ataba tukufu imepokea viongozi wengi wa mkoa wa Karbala na raia wa kawaida waliokuja kutoa salam za sikukuu ya Idul-adh-ha, na kumuomba Mwenyezi Mungu alitunuku taifa la Iraq amani na utulivu.

Muheshimiwa katibu mkuu amemuomba Mwenyezi Mungu akubali ibada za watu wote, alinde taifa la Iraq na watu wake, alitunuku Amani na utulivu, akaonyesha kufurahishwa kwake na watu waliokuja kutoa pongezi za sikukuu na akawatakia kheri nyingi na Baraka.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: