Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini, amempokea katibu mkuu wa Atabatu Husseiniyya Sayyid Hassan Rashidi Al-abaaiji na kupena pongezi za Idul-adh-ha.
Ugeni kutoka Atabatu Husseiniyya umefanya ziara katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kisha ukatoa pongezi za Idul-adh-ha kwa wahudumu wa malalo hiyo takatifu, katika mapokezi hayo pamoja na katibu mkuu wameshiriki wajumbe wa kamati kuu, marais wa vitengo na viongozi wengine.
Wamepeana pongezi za sikukuu ya Idul-adh-ha na kumuomba Mwenyezi Mungu arudishe tukio hili na taifa letu likiwa katika Amani na usalama.
Atabatu Abbasiyya imepokea viongozi mbalimbali wa mkoa wa Karbala na raia wa kawaida waliokuja kutoa pongezi za sikukuu hii tukufu.