Makumbusho ya Alkafeel imepokea wageni wengi katika siku za Idul-adh-ha

Makumbusho ya Alkafeel katika Atabatu Abbasiyya imepokea idadi kubwa ya mazuwaru kutoka ndani na nje ya Iraq katika siku ya Idul-adh-ha.

Idara ya makumbusho ya Alkafeel imesema kuwa milango ya makumbusho ilibaki wazi kuanzia asubuhi hadi jioni, katika siku zoto za Idhul-adh-ha, ili kutoa nafasi kubwa zaidi kwa watu waliopenda kuja kutembelea makumbusho hiyo.

Mazuwaru wamefurahishwa na malikale za thamani na adimu zilizopo ndani ya makumbusho, zinazo onyesha utukufu wa turathi za kitamaduni na kidini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: