Kitengo cha ukanda wa kijani kibichi katika Atabatu Abbasiyya, kimefungua kituo cha kutoa huduma za afya bure kwa familia zinazotembelea eneo hilo.
Kiongozi wa kituo hicho Sayyid Haitham Twaiy amesema “Kufuatia kuingia kwa sikukuu ya Idhul-adh-ha, idara ya matabibu imefungua kituo cha afya kinachotoa huduma bure kwa familia zinazotembelea viwanja vya ukanda wa kijani”.
Akaongeza kuwa “Kituo kinatoa huduma ya kwanza, kisha mgonjwa anapelekwa kwenye hospitali ya karibu na eneo hili kwa ajili ya matibabu zaidi”.
Akabainisha kuwa “Ufunguzi wa kituo hicho ni sehemu ya mkakati wa utoaji wa huduma za afya katika eneo hili lenye ukubwa wa kilometa 9, huduma za afya zinatolewa kwa msaada wa uongozi mkuu wa kitengo na ushirikiano wa hospitali ya rufaa Alkafeel”.
Eneo la ukanda wa kijani kibichi limetembelewa na idadi kubwa ya familia za watu wa ndani na nje ya mkoa wa Karbala, waliokuja kuburudika katika mazingira tulivu ya kijani kibichi.