Atabatu Abbasiyya tukufu imetoa wito kwa ofisi za maraajii Dini na viongozi wa hauza kuhudhuria kwenye wiki ya Uimamu

Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, umetoa wito kwa ofisi za maraajii Dini na viongozi wa hauza katika mji wa Najafu, wa kuhudhuria kwenye wiki ya Uimamu kimataifa awamu ya tatu.

Wiki ya Uimamu inasimamiwa na Atabatu Abbasiyya chini ya kauli mbiu isemayo (Utume na Uimamu ni vitu viwili visivyo tofautiana), na anuani isemayo (Usia wa Maimamu ni muongozo na taqwa), sambamba na Idulghadiir Al-Agharu, kongamano litaanza mwezi 17 Dhulhijjah 1446h, sawa na tarehe 14/06/2025m kwa ushiriki mkubwa wa watu kutoka nchi za kiarabu na kiajemi.

Makamo rais wa kitengo cha mahusiano katika Ataba tukufu, Shekhe Muhammad Jawaad Salami amesema “Ataba imetoa mualiko kwa ofisi za Maraajii Dini na viongozi wa hauza katika mji wa Najafu kuhudhuria wiki ya Uimamu” akabainisha kuwa, “mialiko imepokewa kwa furaha na waalikwa”.

Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia wiki ya Uimamu, huangazia mambo tofauti kuhusu Ahlulbait (a.s) na kubainisha umuhimu wa muongozo wao katika kupambana na changamoto za ulimwengu wa sasa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: