Idhaa ya Alkafeel chini ya ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya imetangaza shindano la (kiapo cha mbingu) katika kuadhimisha Idul-Ghadiir.
Shindano linalenga kuimarisha uwelewa wa kidini na mafundisho ya Ahlulbait (a.s).
Shindano ni maalum kwa wanawake tu, siku ya mwisho kuwasilisha majibu ni Jumamosi 17 Dhulhijjah 1446h sawa na tarehe 14/06/2025m, iwapo majibu yatafanana watachaguliwa washindi watatu kwa njia ya kupiga kura.
Zawadi zitatolewa katika idara ya idhaa ya Alkafeel ghorofa ya tano kwenye jengo la kituo cha Swidiqatu-Twahirah (a.s) lililopo katika mtaa wa Mulhaq.