Mji mtukufu wa Karbala unapokea idadi kubwa ya watu wanaokuja kufanya ziara katika malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuhuisha utii kwa Ahlulbait (a.s).
Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa utaratibu maalum wa utoaji huduma, unahusisha ulinzi, afya, kuongoza matembezi ya mazuwaru mbele ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na zinginezo.