Kitengo cha usafiri kimetangaza utayali wake wa kubeba washiriki wa wiki ya Uimamu kimataifa awamu ya tatu

Kitengo cha usafiri katika Atabatu Abbasiyya kimejiandaa kubeba washiriki wa wiki ya Uimamu kimataifa awamu ya tatu.

Wiki ya Uimamu inasimamiwa na Atabatu Abbasiyya chini ya kauli mbiu isemayo (Utume na Uimamu ni vitu viwili visivyo tengana) na anuani isemayo (Usia wa Maimamu ni muongozo na uchamungu), kufuatia Idul-Ghadiir, hafla itaanza tarehe 17 Dhulhijjah 1446h sawa na tarehe 14/06/2025m, kwa ushiriki wa nchi za kiarabu na kiajemi.

Makamo rais wa kitengo Sayyid Adnani Abbasi amesema “Kitengo kimeandaa mkakati maalum wa kubeba watafiti na wageni wanaoshiriki kwenye wiki ya Uimamu kimataifa awamu ya tatu katika mkoa wa Karbala na Najafu”.

Akaongeza kuwa “Wahudumu wa kitengo cha usafiri wameandaa gari zinazohitajika kutekeleza jukumu hilo”.

Atabatu Abbasiyya kupitia wiki ya Uimamu huangazia mambo tofauti yanayohusu Ahlulbait (a.s), na kubainisha fikra na mwenendo wao katika kutatua changamoto za ulimwengu wa sasa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: