Makamo rais wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya Sayyid Muhammad Twarafi amesema kuwa: Watu wa Karbala kwa kushirikiana na Atabatu Abbasiyya wamezowea kuhuisha Idul-Ghadiir mbele ya malalo ya Imamu Ali (a.s) katika mji wa Najafu.
Akaongeza kuwa, Atabatu Abbasiyya imeandaa mambo yote muhimu, ikiwa ni pamoja na gari za kubeba mazuwaru kwenda na kurudi”, akasema: Hafla imepambwa na qaswida, mashairi na tenzi katika mazingira yaliyojaa furaha ndani ya malalo ya Imamu Ali (a.s), imekua ni kawaida kwa watu wa Karbala kuadhimisha kwa mwaka wa nne mfululizo.
Maukibu ya watu wa Karbala huadhimisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s).