Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake, chini ya ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya, imefanya program ya kuadhimisha Idul-Ghadiir katika mkoa wa Karbala.
Program imehusisha onyesho la igizo lenye anuani isemayo (Kuchukua ahadi), program imefanywa katika kituo cha Swidiqatu Twahirah (a.s) chini ya Ataba tukufu na sardabu ya Imamu Mussa Alkadhim ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maadhimisho hayo yamepambwa na shindano la kitamaduni na kidini kwa ushiriki wa mazuwaru wa malalo takatifu, kwa lengo la kuhuisha mafundisho ya Ahlulbait (a.s) sambamba na Idul-Ghadiir tukufu.