Ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya umetembelea mazuwaru wa kiirani waliopo Karbala

Ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya umetembelea mahujaji wa Iran waliopo Karbala, kutokana na kushindwa kwenda nchini kwao.

Kiongozi wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Jawadi Hasanawi amesema “Ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu umetembelea mahujaji wa Iran waliopo mkoani Karbala, baada ya kumaliza ibada ya Hijja katika nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu”.

Akaongeza kuwa “Ugeni huo umeenda kwa lengo la kutoa msaada kwa mahujaji hao, baada ya kushindwa kurudi nchini kwao kutokana na vita inayoendelea kwa sasa”.

Akabainisha kuwa “Ugeni umewapongeza kwa kufanikiwa kufanya ibada tukufu ya Hijja, kisha ukasikiliza mahitaji yao na kuahidi kuwahudumia kwa kila watakacho hitaji”.

Mahujaji wameishukuru Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa kazi kubwa wanayofanya ya kuhudumia mazuwaru na kutoa misaada kwao kwa kila wanacho hitaji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: