Ofisi ya Marjaa Dini mkuu wa kidini imerudia kulaani mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Iran

Ofisi ya Marjaa Dini mkuu Sayyid Ali Husseini Sistani imetoa tamko la kulaani mashambulizi ya kijeshi yanayo endelea dhidi ya jamhuri ya kiislamu ya Iran.

Ifuatayo ni nakala ya tamko:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu

Marjaa-Dini mkuu katika mji wa Najafu analaani kwa nguvu kuendelea kwa mashambulizi ya kijeshi dhidi ya jamhuri ya kiislamu ya Iran pamoja na kuendelea kuwalenga viongozi wakuu wa kidini na kisiasa katika nchi hiyo, anatahadharisha hatari ya kuendelea jinai hizo -ambazo ni kinyume na misingi ya kidini na kimaadili na uvunjifu wa sharia za kimataifa- jambo hilo litakua na matokeo mabaya sana katika ukanda huu, huenda likafikia hatua isiyoweza kuzuilika na kutokea mzozo mkubwa utakao sababisha hasara kubwa kwa wote.

Tunatoa wito kwa taasisi zote za kimataifa, hususa nchi za kiislamu zifanye kila ziwezalo kusimamisha vita na kutatua mzozo uliopo kwa njia za haki na amani kuhusu swala la nyukilia la Iran kwa kuzingatia kanuni za kimataifa.

(19/06/2025) sawa na (22 Dhulhijjah 1446h).

Ofisi ya Sayyid Sistani – Najafu Ashrafu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: