Makamo rais wa kitengo Sayyid Zainul-Abidina Quraishi amesema “Wahudumu wa kitengo cha kusimamia haram tukufu wameanza kuosha kubba na minara katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ikiwa ni sehemu ya kujiandaa na mwezi mtukufu wa Muharam na shughuli ya kubadili bendera, kwa kupandisha bendera nyeusi katika usiku wa kwanza wa mwezi wa Muharam”.
Akaongeza kuwa “Uoshaji unafanywa kwa umaridadi na umakini mkubwa, inatumika ngazi maalum iliyopo ndani ya Ataba tukufu, inayorahisisha kufanya kazi kwa usalama zaidi”.
Akabainisha kuwa kazi itafanywa kwa siku nne, siku mbili kuosha kubba tukufu na siku mbili zingine kuosha minara miwili, siku ya kwanza katika kila hatua itakua yakuweka ngazi, ukizingatia kuwa kazi hiyo inahitaji umakini wa hali ya juu.