Makamo rais wa kitengo Sayyid Habibu Dahashi amesema “Wahudumu wetu wanatoa huduma mbalimbali kwa mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), ikiwa ni pamoja na kutandika mazulia kila siku, kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili, kwa lengo la kuwawezesha mazuwaru kuswali, kusoma Qur’ani, kusoma dua na ziara”.
Akaongeza kuwa “Wahudumu wanafanya usafi kila siku na kwenda kutupa taka nje ya mji kwa kutumia mitambo maalum”.
Akasema “Idara imeweka madeli ya maji, feni za kawaida, feni za kunyunyiza maji na viyoyozi 30 kwa lengo la kupoza hewa na kupunguza kiwango cha joto”.