Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imefanya hafla ya usomaji wa Qur’ani kwenye wilaya ya Husseiniyya jijini Baghdad.
Hafla ya usomaji wa Qur’ani tukufu imeandaliwa na Maahadi ya Qur’ani chini ya Majmaa ni sehemu ya kuadhimisha Idul-Ghadiir.
Hafla imepambwa na wasomaji wakuu wawili ambao ni Nadhiri Atwani na Muhammad Hamrani, ikafuatiwa na ujumbe kutoka kwa muwakilishi wa Marjaa-Dini mkuu Shekhe Kamali Fartusi, ametoa pongezi kutokana na mnasaba huo mtukufu.
Hafla imehusisha usomaji wa mashairi na qaswida kutoka kwa Karaar Saaidiy, kuadhimisha Idul-Ghadiir.