Uwanja wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) asubuhi ya Ijumaa, umeshuhusia kundi kubwa la mazuwaru wakisoma dua Nudba.
Dua Nudba imesomwa katika mazingira tulivu kwa ushiriki wa mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa mazingira muwafaka kwa kuweka vitabu na kutoa huduma za lazima kwa mazuwaru.