Makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Abbasi Mussa Ahmadi, amesema wanalenga kulea vijana kwa kufuata maelekezo ya Qur’ani tukufu.
Ameyasema hayo alipohudhuria hafla ya kufunga semina ya Qur’ani tukufu iliyosimamiwa na Ataba takatifu.
Akafafanua kuwa, Semina hii ni muendelezo wa semina zilizoanza kufanywa kwa zaidi ya miaka kumi iliyopita, zaidi ya wanafunzi elfu 60 kutoka mikoa 11 ya Iraq, wamenufaika na semina hizi.
Akasema kuwa Ataba tukufu inafanya kila iwezalo kulea vijana kwa kufuata mafundisho ya Qur’ani tukufu na kuwalinda na changamoto za mitandao ya kijamii kwa kuanzisha program mbalimbali za kidini.
Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia semina za Qur’ani katika majira ya kiangazi, inatarajia kutendeneza kizazi cha watu wanaopenda kitabu cha Mwenyezi Mungu, chenye kushikamana na mafundisho ya Dini na mwenendo wa Ahlulbait (a.s)